Uchaguzi Uingereza 2017: Mbwa wafika kwa wingi vituoni

Screen grab of tweet by @kcatclarke Haki miliki ya picha Twitter@kcatclarke
Image caption Fionn, Luna na Roby wakiwa kituoni wamiliki wao walipoenda kupiga kura Cumbria

Wapiga kura walipokuwa wanafika vituoni kupiga kura Uingereza, mbwa wa kila aina hawakuachwa nyuma.

Na punde si punde, watu walianza kugundua kwamba wanyama hao walikuwa wengi sana ajabu, na kitambulisha mada cha #DogsAtPollingstations (Mbwa vituo vya kupigia kura) kikaanza kuvuma mitandaoni.

Kando na mbwa, kunao watoto, paka na hata nungunugu walionekana na kuvutia watu vituoni.

Haki miliki ya picha Twitter/@SAMiCURE
Image caption Phoebe alisubiri nje ya kituo cha kura Manchester

Wengi walipakia picha za mbwa wao mtandaoni Alhamisi asubuhi na katika kipindi cha saa mbili za kwanza baada ya vituo kufunguliwa, ujumbe 8000 kuhusu mbwa ulikuwa umepakiwa mtandaoni.

Mtindo kama huo ulionekana katika uchaguzi wa mitaa mwezi uliopita, kura ya maoni kuhusu kujiondoa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya na wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mwaka huu, Twitter hata walitoa kibonzo cha mbwa akiwa amevalishwa bendera ya Uingereza.

Twitter walishirikiana na wakfu wa The Dogs Trust kutetea kuwepo kwa mazingira bora ya mbwa kwenye vituo vya kupigia kura.

Haki miliki ya picha Twitter/@DachshundOtto
Image caption Otto na Ava wavumilia kibaridi kikali asubuhi katika kituo cha kupigia kura Hampshire
Haki miliki ya picha Twitter/@TheSpeer7
Image caption Max akiwa Tamworth, Staffordshire alionekana kutatizwa na upweke kiasi
Haki miliki ya picha Twitter/@Thefpl_vet
Image caption Si mbwa pekee waliofika vituoni kwa njia ya kipekee. Hapa mbwa Finlay & Ivy wanasubiri nje ya kituo cha polisi wakiwa na watoto wawili, Lexi wa miaka miwili na Owen wa mwaka mmoja katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Whinstone, Ingleby Barwick.
Haki miliki ya picha Peter Maude
Image caption Skye alihakikisha kwamba mpiga picha anapata picha yake nzuri eneo la Essex
Haki miliki ya picha Twitter/@falcoretweets
Image caption Lakini Hugo aliyekuwepo kituoni Nottingham alionekana kutatizwa na mwasho...

There was an interruption when an unexpected guinea pig popped up.

Haki miliki ya picha @MxJackMonroe
Image caption Nungubandia buyu kwa jina Sergeant Pepper, anayefahamika pia kama 'The Wig' alihakikisha nungubandia pia hawaachwi nje.

Lakini mbwa bado walikuwa ndio wengi.

Haki miliki ya picha Deli
Image caption Deli wa aina ya dachshund akiwa London magharibi alihakikisha anamwacha mmiliki wake apige kura kwa faragha
Haki miliki ya picha Twitter/@jodiedoubleday
Image caption Two-year-old Romanian rescue Marlowe wa asili ya Romania na mwenye miaka miwili alikuwa kituoni Canterbury, Kent
Haki miliki ya picha Twitter/@DrRJWalker
Image caption Digby almaarufu Mr Woofs alifika Leicester kutekeleza majukumu yake mbele ya umma kwa kuwa nadhifu na 'mstaarabu'
Haki miliki ya picha Georgie
Image caption Mtazame hapa Bruce wa aina ya Dalmatian aliyesubiri mmiliki wake kwa hamu Derbyshire
Haki miliki ya picha Twitter/@pedventurelurcher
Image caption Ped mbwa wa aina ya Lurcher alionekana kuangazia zaidi kucheza na kujigaragaza juu ya nyasi Surrey.
Haki miliki ya picha Twitter/@H_Ingram
Image caption "Mbona mwaingia huko?" anaonekana kushangaa Mavis akiwa Bury, Lancashire

Baadhi ya mbwa aina ya Pooch hawakuweza kufika vituoni, lakini wanaonekana kutotaka kuachwa nje:

Haki miliki ya picha Twitter/@Mansehound
Image caption Wamiliki wa Sirius The Dog eneo la Knockbain, Scotland walipiga kura yao mapema kupitia posta. Lakini hawakutana kuachwa nje katika kusambaza picha za mbwa

Kuliwepo hata hivyo na wanapaka, na kitambulisha mada ya #catsatpollingstations (paka vituoni) pia kilivuma kiasi.

Haki miliki ya picha Twitter/ @cbowyercreative
Image caption Paka hutu alionekana Clare Bowyer eneo la Colburn, North Yorkshire. Hakukuwepo na mbwa karibu.

Hata nungunungu huyu kwa jina Friday alitaka kushiriki Hemel Hempstead.

Haki miliki ya picha Toni Lambert
Image caption Nungunungu kwa jina Friday katika kituo cha kura Hemel Hempstead

Na farasi je? Walikuwepo pia.

Haki miliki ya picha Twitter/@FontwellPark
Image caption Sunset Skye akiwa Sussex Magharibi
Haki miliki ya picha Twitter/ @kazzimazzi
Image caption Na mwisho kabisa kulikuwa na kondoo na mwanakondoo wake kituo cha kura cha Melness, Sutherland.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii