Iran 'yapuuzilia mbali' taarifa ya Trump kuhusu shambulio la Tehran

Wanajeshi wa Iraq wazingira majengo ya Bunge wakati wa shambulio
Image caption Wanajeshi wa Iraq wazingira majengo ya Bunge wakati wa shambulio

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Iran, amepuuzilia mbali na kutaja kama "isiyokubalika" taarifa ya White House siku ya Jumatano, pale Tehran iliposhambuliwa na magaidi; taarifa hiyo ilisema kuwa Tehran ni "wafadhili wa ugaidi".

Rais Trump alisema kuwa anawaombea manusura, na akaongeza kuwa "mataifa yanayofadhili ugaidi, yamo kwenye hatari ya kushambuliwa na magaidi hao hao waliowafadhili".

Lakini Javad Zarif, amesema kuwa Iran "imekatalia mbali madai hao ya kuwepo urafiki" na kudai kuwa kundi la Islamic State linaungwa "mkono na wateja wa Marekani".

Iran imemnyonga mwanasayansi kwa usaliti

Ahmadinejad azuiwa kuwania urais Iran

Watu 13 walifariki katika shambulio hilo.

Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki pamoja na wahanga wa kujitoa kufa, walilenga bunge la taifa hilo na jumba lilimo kaburi la mwaanzilishi wa taifa hilo la kiislamu Ayatollah Khomeini, katika mashambulio mawili ambayo hayakutarajiwa, Jumatano asubuhi.

Image caption Ramani hakiki ya maeneo mjini Tehran

Iran inasema washambuliaji, ambao wote waliuwawa, walikuwa raia wa Iran ambao walijiunga na wanamgambo wa IS.

Kundi hilo aidha, limetoa vitisho vya kushambulia zaidi utawala wa Iran, ambao ni wa waislamu wa Kishia.

Katika taarifa ya awali kwenye mtandao wa kijamii wa tweeter, Bwana Zarif alionekana kulaumu wapinzani wao katika anda hiyo kuwa ndio waliohusika na shambulio hilo huku akisema: "walioufadhili ugaidi huu wana njama za kutaka kuleta vita katika ardhi yetu.

Waislamu Wa-Sunni-ndio wanaoongoza Saudi Arabia - mshirika mkuu wa Marekani ilihali kwa upande mwingine Waislamu wa Shia-ndio wanaotawala Iran, na ni mahasimu wakuu wawili katika kanda hiyo ya mataifa ya kiislamu.

Mamlaka kuu ya Saudia, imekuiwa ikiwapa pesa na silaha makundi yenye misimamo mikali ya kiislamu yenye nia ya kuuangusha utawala wa Rais wa Syria Bashar al-Assad - Mshirika wa dhati wa Iran.

Mashirika mengi ya utoaaji misaada na watu mashuhuri wamekuwa wakilaumiwa kwa kufadhili wasunni wenye misimamo mikali ya kidini kote katika mataifa hayo ya milki ya kiarabu kwa miongo miwili iliyopita.

Mwezi uliopiota, Rais Donald Trump, alizuru Saudi Arabia na kutoa hotuba ya kuilaumu hadharani Iran nkwa kuyumbisha amani katika kanda hiyo.