Matokeo ya Uchaguzi 2017 kwa kifupi: Maeneo muhimu kwa mtazamo

Matokeo hayo yakingaa juu ya Jumba la Habari - bbc
Image caption Makadirio ya matokeo ya uchaguzi baada ya upigaji kura

Makadirio ya pamoja ya BBC, ITV na Sky kutokana na utafiti wa baadhi ya upigaji kura yanaonesha viti 322 vitanyakuliwa na chama cha Conservatives, idadi ambayo itakuwa viti 9 chini ya viti vilivyonyakuliwa na chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Chama cha Labour kitapata viti 261, ongezeko la wabunge 29, nacho chama cha SNP kipoteze wabunge 24.

Chama cha Lib Dems kitajiongezea wabunge watano zaidi zaidi na kufikia wabunge 13, Plaid Cymru kikisalia na wabunge 3 pekee.

Greens watakuwa na mbunge mmoja nao UKIP wabaki bila mbunge yeyote.

Vyama hivyo vingine vidogo vitakuwa kwa jumla ya wabunge 18.

Matokeo ya utafiti wa baada ya uchaguzi uliofanywa kwa pamoja na BBC, ITV na Sky yanaonesha hakuna chama kitakachopata wingi wa wabunge katika Bunge la Commons.

Makadirio hayo yanaonesha kuwa, chama cha Conservatives kitaimarika kwa kiasi fulani, kuliko ilivyotabiriwa kwenye matokeo yaliyobashiriwa ya baada ya upigaji kura, lakini kitamaliza chini kidogo ya idadi ya wabunge wanaohitajika kuunda serikali kwa wingi wa wabunge.

Haki miliki ya picha PA

Please enable Javascript to view our results map