Waasi wa Sudan wakiri kuhusika na shambulio la mabasi

Waasi wa Sudan Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wa Sudan Kusini

Waasi wa Sudan Kusini wamesema walihusika katika shambulio la msafara wa mabasi yaliokuwa yakielekea Juba lililosababisha vifo vya watu 14.

Msemaji wao ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kikosi hicho cha waasi kilikuwa kinalenga kikosi cha serikali.

Lam Paul Gabriel aliongeza kwamba wanajeshi hao walikuwa wanawasindikiza raia na waliuawa katika kisa cha ufyatulianaji wa risasi.

Bwana Lam amesema wapiganaji wake waliwaua watu 40 , ikiwemo makanali wawili katika shambulio lililo tumia roketi ya propela ya Gruneti.

Lakini Msemaji wa polisi wa Sudan Kusini , Daniel Justin Boulogne, amesema ni watu 14 waliouawa.

Radio ya Sudan Kusini ya Eye imechapisha kwenye mtandao wake wa Tweeter kuhusiana na idadi kamili ya watu waliouawa.