Farmajo asema atalipiza kisasi kwa kundi la al-shabab

Farmajo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Somalia Farmajo ameahidi kuwa mkali kwa kundi la al-Shabab

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amesema al-Shabab hawataepuka kwa kutekeleza shambulio la siku ya Alhamisi katika kambi ya jeshi lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 38 , Shirika la habari la Reuters limeripoti.

Al- Shabab imesema wanajeshi 61 waliuawa katika shambulio la asubuhi lililotokea karibu kilomita 70 kutoka Kaskazini Mashariki mwa Bosaso, lakini maafisa wa nchi hiyo wamesema hiyo sio idadi kamili ya vifo.

Katika taarifa , iliyonukuliwa na vyombo vya habari tofauti , Bwana Farmajo amesema:

''Hii ni mara nyengine inadhibitisha kwamba maadui wanaotuandama ni hatari, na inasababisha ukosefu wa amani katika nchi yangu na wanastahili kukabiliwa kwa njia zozote zile. Tutawaonyesha hatuna huruma kwa kukabiliana nao.''

Jimbo la Puntland limekuwa likikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa al-Shabab, lakini shambulio hili la sasa limetajwa kuwa baya zaidi katika siku za hivi karibuni.

Mada zinazohusiana