Mabaki ya binadamu 'wa kwanza' yapatikana Morocco

Ujenzi wa kwanza wa kisukuku cha awali zaidi cha binadamu kutoka Jebel Irhoud (Morocco) kulingana na nakala za tomografia. Haki miliki ya picha PHILIPP GUNZ/MPI EVA LEIPZIG
Image caption Ujenzi wa kwanza wa kisukuku cha awali zaidi cha binadamu kutoka Jebel Irhoud (Morocco) kulingana na nakala za tomografia.

Uchunguzi umebainisha kuwa dhana ya kuwa asili ya binadamu wa kwanza ni kutoka Afrika ya Mashariki zaidi ya miaka laki mbili iliyopita sio kweli.

Visukuku vya binadamu watano wa mapema imepatikana Kaskazini mwa Afrika na inaonyesha binadamu wa kwanza aliishi miaka 100,000 zaidi ya vile ilivyodhaniwa.

Prof Jean-Jacques Hublin, kutoka Leipzig, Ujerumani, anasema kuwa ugunduzi huu unaweza "kuandika upya vitabu vya kiada" kuhusu kuibuka kwetu .

"Sio hadithi ya hayo kutokea kwa njia ya haraka katika 'shamba la Edeni' mahali fulani barani Afrika. Ilikuwa ni maendeleo ya taratibu. Kwa hiyo kama kulikuwa na bustani ya Edeni, ilikuwa ni kote kote Afrika.

Prof Hublin alikuwa akiongea katika mkutano wa wanahabari katika chuo kimoja mjini Paris, ambako aliwaonyesha waandishi kisukuku ambacho timu yake ilichimbua katika eneo la Jebel Irhoud, Morocco. Sampuli hiyo ni ya na fuvu, meno na mifupa mirefu.

Mabaki yaliyopatikana katika eneo hilo hapo awali yalisemekana kuwa na miaka elfu 40. Lakini Prof Hubli alikuwa na tashwishi na kwa muda mrefu aliendelea kufanya utafiti katika eneo hilo la Jebel Irhoud na miaka 10 baadaye, anawasilisha ushahidi mpya unaoelezea hadithi tofauti.

Mabaki hii ya sasa inadaiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 300,000 na 350,000 miaka. Na fuvu yake ni ya aina karibu sawa na ya binadamu wa kisasa.

Hadi sasa, mabaki ya binadamu wa kwanza yalikuwa kutoka Ethiopia (kutoka tovuti inayojulikana kama Omo Kibish) , Afrika mashariki na walidaiwa kuwa na umri wa takribani miaka 195,000.

Kabla ya watu wa aina yetu, kulikuwa na aina nyingi tofauti ya binadamu, na kila alikuwa na uwezo na udhaifu tofauti. Na hawa aina mbalimbali ya binadamu, kama vile wanyama wengine, waliendelea kubadili muonekano wao hatua kwa hatua.

Jebel Irhoud inafanana na sehemu kadhaa za kihistoria barani Afrika ambayo ina miaka 300,000. Maeneohaya yana zana sawa na pia ushahidi wa matumizi ya moto.

Mada zinazohusiana