Marekani yazitaka nchi za kiarabu kulegeza kamba kwa Qatar

Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar Haki miliki ya picha EPA
Image caption Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasema kuwa nchi za Ghuba ni lazima zilegeze hatua yao dhidi ya Qatar ambayo inalaumiwa na majirani zake kwa kuunga mkono Ugaidi.

Saudi Arabia, Muungano wa nchi za kiarabu, Misri na Bahrain walikata uhusiano wa usafiri na wa kidiplomasia na Qatar siku ya Jumatatu.

Bwana Tillerson anasema kuwa hatua hiyo inasabisha kuwepo madhara ya kibinadamu.

Licha la kumsifu Emir wa Qatar kwa kupuza uungwaji mkono makundi ya kigaidi, Bwana Tillerson anasema mengi yanahitaji kufanywa.

Naye Rais Trump ameishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na kuitaka ikome

Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar, na hata kudai kuwa alishiriki katika uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia pamoja na nchi zingine.

Ndege za Qatar zilipigwa marufuku ya kutumia anga za baadhi ya majirani zake.

Hatua hiyo ya ghafla ilichukuliwa baada ya msukosuko ambao umedumu miaka kadha kati ya Qatar na majirani zake wa Ghuba.

Image caption Nchi za Ghuba