Trump: Marekani italinda nchi za NATO

Makao makuu ya NATO Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Makao makuu ya NATO

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa ahadi maalum ya kujitolea kwake katika kufanikisha mkataba wa mataifa ya kujihami ya NATO, ambapo mataifa wanachama huwa yamekubaliana kulinda kila mmoja.

Kuliibuka wasiwasi miongoni mwa mataifa wanachama baada ya rais Trump kukosa kuunga mkono hadharani kipengee cha tano cha mkataba wa NATO, wakati alipozuru makao makuu ya NATO mwezi mei mjini Brussels.

Katika mkutano huo rais Trump alitaka mataifa wanachama kulipa pesa zaidi za kuimarisha ulinzi wa muungano huo.

Hata hivyo hapo jana baada ya mkutano na rais wa Romania , Klaus Iohannis, bwana Trump alisema, nikimnukuu 'kwa hakika tuko hapa kulinda'.