Ethiopia kuishiwa na chakula ifikapo mwezi ujao

Pia ukame uliikumba Ethiopia mwaka uliopita Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pia ukame uliikumba Ethiopia mwaka uliopita

Ethiopia itaishiwa na chakula cha dharura kwa watu milioni 7.8 wanaokumwa na ukame ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, Umoja wa Mataifa umeonya.

Mashirika ya kutoa misaada na serikali yameotoa wito wa msaada, licha ya hofu ya kuwepo majanga mengine kote duniani.

Njaa kaskazini mashariki mwa Nigeria, Sudan Kusini Yemen na Somalia yametajwa kuwa majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani tangu mwaka 1945.

Lakini Ethiopia pia inakumbwa na hali ngumu kufuatia ukosefu wa mvua.

Huku serikali ikijikakamua kukabiliana na ukame kuliko miaka ya nyuma, bado haina pesa kuweza kutatua tatizo hilo peke yako.

Ilikuwa imetenga dola milioni 381 kwa miaka miwili iliyopita lakini haina uwezo wa kuendelea kwa mwaka wa tatu.

Hii imeiacha Ethiopia katika hali mbaya, kwa mujibu wa Jonh Aylief wa shirika la mpango wa chakula duniani.