Mazungumzo ya "kigaidi" yasababisha ndege kutua ghafla Ujerumani

The Easyjet plane Haki miliki ya picha Dave Hargreaves
Image caption Abiria wote 151 waliaondelwa na safari za ndege kufutw kwa muda wa saa tatu

Ndege iliyokuwa safarini kutoka Slovania ikielekea Uingereza ilitua kwa ghafla baada ya rubani kujulishwa kuhusu mazungumzo ya kutiliwa shaka yaliyokuwa na matamshi ya kigaidi.

Wanaume watatu raia wa Uingereza waliokamatwa baada ya ndege ya kampuni ya Easyjet kuelekezwa mji wa Cologne, Ujerumani siku ya Jumamosi wanahojiwa.

Abiria wote 151 waliaondelwa na safari za ndege kufutwa kwa muda wa saa tatu.

Mfuko uliokuwa unamilikiwa na wanaume hao ulilipuliwa na polisi.

Msemaji wa uwanja wa ndege wa Cologne alisema kuwa rubani alikuwa amejulishwa kuhusu mazungumzo ya kutiliwa shaka kwenye ambapo aliamua kutua kwa ghafla.

Watu 9 walitibiwa baada ya kushuka kutoka kwa ndege wakitumia milango la dharura ya ndege hiyo Airbus 319.

Kampuni ya Easyjet ilisema kuwa rubani alichukua uamuzi wa kutua kuruhusu ukaguzi wa kiusalama kufanyika.

Haki miliki ya picha Dave Hargreaves
Image caption Watu 9 walitibiwa baada ya kushuka kutoka kwa ndege wakitumia milango la dharura ya ndege hiyo Airbus 319.