Wahamiaji 112 wakamatwa Mexico wakielekea Marekani

Wahamiaji hao wanasema hulipa fedha nyingi kuweza kufika Marekani
Image caption Wahamiaji hao wanasema hulipa fedha nyingi kuweza kufika Marekani

Mamlaka nchini Mexico imegundua wahamiaji 112 wakiwemo watoto wakiwa hai nyuma ya gari ambalo lilikua linaelekea nchini Marekani.

Maofisa wa serikali wanasema kuwa gari hilo lilikamatwa wakati likiwa sehemu inayounganisha miji ya Chiapas na Tabasco.

Wahamiaji hao wanasemekana kutoka nchi za Guatemala, El Salvador, Honduras na Ecuador.

Maelfu ya raia wa Amerika ya Kati hujaribu kutoroka nchi zao na kuingia Marekani kuimbia umaskini na vita.

Dereva wa gari hilo amekamatwa.