Ndege iliyotoboka shimo kwenye injini yatua salama Australia

Ndege hiyo ilitua salama

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Ndege hiyo ilitua salama

Ndege moja ya shirika la China Eastern Airlines ililazimika kurudi mjini Sydney Australia baada ya kupatwa na hitilafu wa mitambo ambayo ilisababisha shimo sehemu ya injini ya ndege hiyo.

Ndege ya MU736 ilikuwa safarini kutoka Sydney ikilekea Shanghai China lakini rubani akaripoti kuhusu matatizo kwenyr injini katibu saa moja baada ya ndege kuanza safari.,

Abiria waliambia vyombo vya habari kuwa walihisi harufu na kitu kinachochomeka ndani ya ndege.

Ndege hiyo aina ya Airbus A330 ilitua salama na hakukuwa na ripti zozote za majeruhi.

Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha shimo kubwa upande wa injini.

Abiria kadha walisema kuwa walisikia sauti kubwa ikitokea injini ya upande wa kushoto muda mfupi baada ya ndege kupaa.

Abiria mmoja aliambia shirika la Seven News Network, "ghafla tukaskia sauti hii...kisha tukahisi haribu ya kuchomeka."

Chanzo cha picha, Reuters TV

Maelezo ya picha,

China Eastern Airlines lililisema kuwa abiria watapewa ndege nyingine