Puerto Rico yapiga kura kujiunga na Marekani

Puerto Rico Governor Ricardo Rossello (C) and his wife Beatriz Rossello (R) greet voters on 11 June, 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gavana wa Puerto Rico Ricardo Rossello (katikati) na mkewe Beatriz Rossello (kulia)

Himaya ya Marekani ya Puerto Rico imepiga kura ya kuomba bunge la Congress kuifanya kuwa jimbo la 51 la Marekani.

Zaidi ya asilimia 97 ya wapiga kura walipendelea kujiunga na Marekani badala ya kuwa huru au kuwa himaya tu ya kujisimia.

Hata hivyo asilimia 23 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura licha ya upinzani kususia kura hiyo.

Hata hivyo uamuzi wa mwisho hauko mikononi mwao bali kwa Congress.

Kura hiyo ya maoni ya mwaka 2017 ilitishwa na serikali baada ya kushuhudiwa kwa hali ngumu ya kiuchumi ambayo wengi wanadai kuwa imetokana na hali ya sasa ya Puerto Rico ambayo ni nusu kati ya kuwa na uhuru au himaya linalojisimamia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kulikuwa na maandamano ya kupinga Puerto Rico kwa taifa la 51