Chama cha rais Emmanuel Macron kujinyakulia viti vingi vya bunge

Ufaransa
Image caption chama kipya cha rais Emmanuel Macron kujinyakulia viti vingi vya bunge

Mzunguko wa kwanza wa kura za maoni katika uchaguzi wa bunge nchini Ufaransa unaonyesha dalili za chama kipya cha rais Emmanuel Macron kujinyakulia viti vingi vya bunge.Makadirio yanaonyesha kuwa chama hicho kinaweza kupata viti 440.

Hata hivyo makadirio ilikuwa ni kupata asilimia 50 tu jambo ambalo lilimpatia wasi wasi mkuu wa chama cha republicans Francois Baron

"Kiwango cha idadi kubwa ya wasiopiga kura hakijawahi kutokea tangu 1958, jambo linaloonyesha mgawanyiko mkubwa katika jamii ya Ufaransa kwa sasa.Mgawanyiko huu ulionekana wazi katika mzunguko wa kwanza wa uchaguzi wa Rais. Katika mzunguko wa kwanza wa uchaguzi wa rais karibia kila raia mmoja wa Ufaransa kati ya wawili alichagua msimamo mkali kisiasa.Katika mzunguko wa pili wapiga kura milioni 16 walikataa kuchagua kati ya Emmanuel Macron na chama cha National Front kwa ama kutojitokeza kupiga kura ama kupiga kura zilizoharibika. Safari hii idadi ya wapiga kura imeendelea kupungua jambo linalotia mashaka. "

Image caption mgombea wa Urais Marine Le Pen

Upande wa Soshalist huenda ukapata pigo kubwa,kwa ni inaonekana chama cha Front National cha aliyekuwa mgombea wa Urais Marine Le Pen,huenda kikapata viti vingi Zaidi ya viwili walivyo navyo kwa sasa.Hata hivyo amelaumu mfumo wa uchaguzi wa Urfaransa.

''Kiwango hiki cha kutisha cha kushuka kwa idadi ya wapiga kura ni lazima kuzue maswali dhidi ya mfumo huu wa upigaji kura,kunakosababisha mamilioni ya wapiga kura kutojitokeza,na inaonyesha kuwa hawana wagombea sahihi wanaowataka kati ya waliopo''