Muuza ndizi wa miaka 94 aliyeporwa Indonesia achangiwa pesa

Suratman Haki miliki ya picha Facebook: TommyReza Chokolatoz
Image caption Kind-hearted Indonesians reacted to Mr Suratman's plight in a strong show of support

Watu nchini Indonesia wameungana kumsaidia mzee mmoja muuza ndizi ambaye anasema kuwa aliiporwa zaidi ya rupiah milioni 1 au dola 80

Suratman mwenye umri wa miaka 94, aliombwa na dereva mmoja aingie kwenye gari lake ili auze matunda.

Akiwa ndani ya gari hilo wanaume hao walimlazimisha Bwana Suratman kutoa pesa zote kwa mfuko, kisha wakamtupa nje na kutoroka kwa gari lao.

Tommy Reza alichapisha video ya Bwana Suratman akiwa mwenye mawazo ambayo imevutia huruma na watu kutoa mchango.

Haki miliki ya picha Facebook: Tommy Reza Chokolatoz
Image caption Mzee Suratman alipoteza pesa zake kwa kundi la wanaume

Kisa hicho kilitokea mkoa wa Jambi katika kisiwa cha Sumtara. Tommy Reza aliambia BBC kuwa alimpata Bwana Suratman akiwa mwenye majonzi.

"Nilikuwa eneo hilo wakati nilimuona mwanamume akipiga kelele akiomba msaada," alisema Reza.

Tangua video hiyo iweke kwenye mitandao ya zaidi ya rupiah milioni 37, zaidi ya dola 2900 zimechangwa.

Gavana wa eneo hilo baadaye alitoa rupiah milioni 5. Kisha bwana Reza akachapisha picha akimkabidhi Suratman pesa hizo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii