Wakazi Nairobi wakimbia na kupakwa rangi kuhimiza amani
Wakazi Nairobi wakimbia na kupakwa rangi kuhimiza amani
Mamia ya wakazi wa Nairobi walihudhuria tamasha la Mbio za rangi Kenya, ambazo lengo lake lilikuwa kukuza amani na utangamano miongoni mwa Wakenya wakati wa uchaguzi.
Mbio hizo ambazo asili yake ni tamasha la Holi nchini India ziliandaliwa kwa mara ya kwanza nchini Kenya kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kudumisha amani mwaka huu wa uchaguzi na pia kusherehekea tofauti na asili mbalimbali za Wakenya.
Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza kuandaa mbio hizo Afrika.