Mamia wakamatwa maandamano ya kupinga serikali Urusi

Tverskaya, Moscow (12 June)
Image caption Polisi wa Fanya Fujo Uone walitumwa kwa wingi Moscow

Polisi wa kupambana na fujo nchini Urusi, wamewakamata na kuwazuilia mamia ya waandamanaji waliokuwa wakipinga madai ya ufisadi katika Serikali ya nchi hiyo.

Maandamano makubwa mno yameshuhudiwa katika miji ya Moscow na St Petersburg, mahali ambapo maelfu ya waandamanaji walijitokeza, huku wengi wao wakipiga kelele kumlaani Rais Vladimir Putin.

Polisi wamemtia mbaroni mwandalizi wa maandamano hayo Alexei Navalny ambaye ni mkosoaji wa serikali na kiongozi mkuu wa upinzani nchini Urusi.

Kiongozi mkuu wa idara ya usalama nchini Urusi, alitaja maandamano hayo kama ya uchokozi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwandamanaji akikamatwa barabara ya Tverskaya, katikati mwa Moscow

Wengi wa waandamanaji walifoka "Putin is a thief!" yaani "Putin ni mwizi" "Russia will be free" yaani "Urusi itakuwa huru!"

Zaidi ya watu 600 wanadaiwa kukamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi wa kupambana na fujo katika mji mkuu Moscow, na wengine 300 wamekamatwa katika mji wa St Petersburg.

Bw Navalny anatazamiwa kumpinga Rais wa Vladimir Putin katika kiti cha Urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Rais Putin hajatangaza rasmi iwapo atawania tena kiti hicho au la.


Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vijana pia walikamatwa mjini St Petersburg

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwanamke huyu alijifunga kitambaa chenye marangi ya bendera ya Urusi
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wengi walikusanyika mjini St Petersburg, mji wa pili kwa ukubwa Urusi

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii