Oman yapeleka chakula Qatar

Baadhi ya makontena yaliyobeba vyakula katika bandari ya Oman
Image caption Baadhi ya makontena yaliyobeba vyakula katika bandari ya Oman

Nchi ya Qatar imefungua huduma za usafiri wa meli kutokea Oman kwa lengo la kukabiliana na vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na majirani zake.

Meli kadhaa zikiwa zimebeba vyakula na bidhaa mbalimbali zimeonekana zikielekea Qatar kutokea bandari mbili zilizopo Oman.

Qatar inategemea uingizwaji wa chakula kutoka nje.

Saudi Arabia, Bahrain na muungano wa Falme za Kiarabu zilizuia uingizwaji wa bidhaa kwenda Qatar wiki chache zilizopita kwa shutuma kuwa nchi hiyo inaunga mkono vitendo vya kigaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Qatar amewasili mjini London na kisha Paris kujadili mgogoro huo.

Wakati hatua ya kuitenga Iran ilianza wiki iliyopita kulikuwa na ripoti za watu kununua chakula kwa wingi wakihofia kuwepo upungufu.

Image caption Qatar huagiza asilimia kubwa ya chakula chake kutoka nchi za nje

Lakini mwishoni mwa wiki bidhaa kutoka Uturuki zilianza kuwasili katika maduka na ndege tano lizosheheni matunda na mbona nazo ziliondoka nchini Iran.

Meli tatu zilizosheheni tani 350 za chakula pia zinatarajiwa kuondoka nchini Iran kuelekea Qatar.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar anasema kuwa asilimia 16 ya chakula chake kilikuwa kinasafirishwa kupitia Saudi Arabia ambayo ilifunga mpaka wake.

Mada zinazohusiana