Serikali ya Venezuela yaongeza ulinzi katika jimbo la upinzani

Kwa miezi miwili polisi wamekuwa wakiwazuia waandamanaji wanaofanya fujo nchi nzima
Image caption Kwa miezi miwili polisi wamekuwa wakiwazuia waandamanaji wanaofanya fujo nchi nzima

Wizara ya mambo ya ndani nchini Venezuela imeongeza ulizni zaidi katika jimbo la Miranda,ambalo linaongozwa na kiongozi wa upinzani nchini humo Henrique Capriles.

Serikali inasema kumekuwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadam katika eneo hilo.

Capriles anasema kuwa kitendo cha wizara kuongeza polisi katika jimbo lake ni masuala ya siasa zaidi ya ulinzi.

Miranda amabayo ni sehemu ya mji mkuu Caracas ni miongoni mwa sehemu zenye maandamano makubwa dhidi ya Rais Nicolas Maduro.

Zaidi ya watu 60 wameuawa katika maandamano hayo yaliyoanza miezi miwili iliyopita.