Kiongozi wa upinzani Urusi atupwa jela kwa kuandaa maandamano

Alexei Navalny (right) speaks after a hearing in a court in Moscow. Photo: 12 June 2017

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha,

Alexei Navalny (kulia) ana nia ya kugombea urais mwaka ujao

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amehukumia kifungo cha siku 30 jela kwa kukiuka sheria baada ya kuandaa maandamano

Alikamatwa nyumbani kwake mjini Moscow siku ya Jumatatu kabla ya kufanyika kwa maandamano ya kupinga ufisadi nchini Urusi.

Mamia ya watu walikamhwa wakati wa maandamano hayo yaliyofanyika kote nchini.

Polisi wa kupamba na maandamano walikuwa wakiwakamata waandamanaji kutoka kwa umati, kwa mujibu wa mwandjshi wa BBC aliyekuweko.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Vijana wakamatwa mjini St Petersburg

Mahakama ya Moscow iltangaza umuzi wake jana Jumatatu na kukataa wito wa mawakili wa Navalny kufuta kesi hiyo.

Kiongozi huyo wa upinzani mwenyr umri wa miaka 42 baadaye alithibitisha hukumu yake katika mtandao wa twitter.

Polisi mjini Moscow wanasema kuwa takriban watu 5000 walishiriki maandamano hayo mjini humo.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mwandamanaji akikamatwa mjini Moscow