Rais wa zamani wa Panama Ricardo Martinelli akamatwa Marekani

Former Panamanian President Ricardo Martinelli. File photo Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ricardo Martinelli anakana madai dhidi yake

Rais wa zamani wa Panama Ricardo Martinelli amakamatwa katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Kikosi cha kudumisha sheria nchini Marekani kinasema kuwa Martinelli mwenye umri wa miaka 65 alikamatwa karibu na nyumbani kwake huko Coral Gables.

Mwaka uliopita Panama ilitoa ombi la kutaka Bwana Martinelli ambaye analaumiwa kwa ufisada na ujasusi wa kisiasa kurudishwa nchini humo.

Bwana Martinelli ambaye aliongoza taifa hilo la Amerika ya kati kutoka mwaka 2009 hadi 2014 anasema kuwa madai hayo yamechochewa kisiasa.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani huko Florida leio Jumanne.

Mwaka 2015 mahaka ya juu nchini Pana iliamrisha bwana Martinelli akamatwe kufuatia shutuma kuwa alitumia pesa za umma kuwafanyia ujasusi zaidi ya watu 150 mashuhuri.

Kati ya watu aliowafanyai ujasusi ni pamoja na viongozi wa mashirika ya umma, wanaharakati, wanasiasa, mawakili na wafanyayibiashara.

Mada zinazohusiana