Watu 4 wapigwa risasi mjini Munich, Ujerumani

Polisi walimpiga risasi na kumjerudi mshambuliaji ambaye sasa yuko kizuizini.
Image caption Polisi walimpiga risasi na kumjerudi mshambuliaji ambaye sasa yuko kizuizini.

Polisi mmoja mwanamke amepigwa risasi kichwani wakati mwamamume mmoja alipampokonya bunduki yake katika kituo kimoja cha treni mjini Munich.

Mwanamke huyo alijeruhiwa vibaya pamoja na watu wawili waliokuwa kando ambao walijeruhiwa awakti wa ufayatuaji huo wa risasi, kwa mujibu wa polisi.

Polisi walimpiga risasi na kumjeruhi mshambuliaji ambaye sasa yuko kizuizini. Polisi wanasema kuwa hakikuwa kisa cha ugaidi.

Oparesheni kubwa ya polisi inaendelea na huduma za usafiri wa reli zimesitishwa

Watu waliokuwa kando pamoja na mshukuwa hakujeruhiwa vibaya

Polisi wanasema kuwa hakuna hatari yoyote kwa umma

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Oparesheni kubwa ya polisi inaendelea na huduma za usafiri wa reli zimesitishwa

Mada zinazohusiana