Nyota wa zamani wa Chicago Bulls arejea Korea Kaskazini

Dennis Rodman mobbed by the press en route to Pyongyang Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dennis Rodman akiongea na waandishi wa habari mjini Beijing akielekea Korea Kaskazini

Aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Dennis Rodman amefanya tena ziara nchini Korea Kaskazini.

Nyota huyo wa zamani wa NBA anafanya ziara ya kibinafsi.

"Ninajaribu tu kufungua mlango," aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege mjini Beijing akielekea nchini Korea Kaskazni.

Aligonga vichwa vya habari baada ya kufanya urafiki na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, wakati wa ziara zake za awali mwaka 2014 na 2014 nchini Korea Kaskazini.

Rodman amemtaja Kim kama rafiki wa maisha.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Marekani inasema kuwa inafahamu ziara yake.

"Tunamtakia mema, lakini timetoa onyo mwa raia wa Marekani na kuwashauri wasisafiri kuenda Korea Kaskazini kwa usalama wao," naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Thomas Shannon, alisema.

Haki miliki ya picha AFP / Getty Images
Image caption Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un na Dennis Rodman wakitaza mpira wa kikapu mwaka 2013

Msukosuko kati ya Marekani na Korea Kaskazini umekuwa mkubwa chini ya utawala wa Rais Donald Trump, ambaye anasema kuwa anahofia mzozo mkubwa huenda ukaibuka kati ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo Trump pia amesema kuwa angependa kukutana na bwana Kim wakati mwema.

Akizungumzaa kwemye uwanja wa ndege, bwana Rodman alisema " Nina furaha kuwa Trump anafarahia sababu kuwa mimi niko hapa na ninajaribu kutimiza kitu fulani ambacho sisi sote tunahitaji.

Bwana Rodman aliuunga mkono kampeni ya Trump.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chicago Bulls, wakati mmoja alimshauri Rais Barack Obama ampigie simu Bwa Kim, akisisitiza kuwa wote walikuwa mashabiki wa mpira wa kikapu.

Hata hivyo ziara zake zinatajwa na vyombo vya habari nchini Marekani kuwa diplomasia ya mpira wa kikapu.

Mada zinazohusiana