Ugonjwa wa Polio wabainika DRC

WHO
Image caption Shirika la Afya duniani, WHO limebaini milipuko miwili ya ugonjwa wa polio nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Shirika la Afya duniani, WHO limebaini milipuko miwili ya ugonjwa wa polio nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Inasemekana kuwa kuna hatari kubwa ya ugonjwa huo kusambaa.

Uwepo wa maambukizi ya ugonjwa huo wa polio umebainika upo katika maeneo ambayo hawakupata kinga ya kutosha.

Maambukizi ya polio yanawashambulia zaidi vijana na athari zake ni kupooza kwa kudumu.

Haki miliki ya picha DRC
Image caption Vijana waathirika zaidi na ugonjwa wa Polio

Licha ya kuwepo kwa kampeni nyingi duniani za kuutokomeza ugonjwa huu lakini bado unasambaa nchini Nigeria, Pakistan na Afghanistan.