Waasi wa FARC wasalimisha asilimia 30 ya silaha zao

FARC Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waasi wa kundi la FARC la Colombia wamesalimisha asilimia 30 ya silaha zao kwa wakaguzi wa umoja wa kimataifa

Waasi wa kundi la FARC la Colombia wamesalimisha asilimia 30 ya silaha zao kwa wakaguzi wa umoja wa kimataifa,kama sehemu ya utekelezaji wa mkataba wa kihistoria wa amani uliosaniwa mwaka jana.

Hata hivyo hatua hiyo inatajwa kuwa ni kuelekea mafanikio ya maridhiano ya Amani nchini humo.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amesema kuwa kuwa hii ni hatua ya kiihistoria kwa mjibu wa mkataba na kwamba ni kusonga mbele katika mipango iliyowekwa.

"Hatimaye,hatua muhimu imefikiwa,kupunguza silaha kwa kundi la FARC,kama tulivyoona,kama ilivyozungumzwa hapa ni hatua ya pili muhimu,asilimia 30kwa siku chache tu tutafikia asilimia 60 na hatimaye asilimia 100 wiki ijayo"

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wajumbe wa kundi la FARC wakikabidhiwa vyeti na Umoja wa mataifa

Kamanda wa kundi la FARC,Pablo Catatumbo,amesema kuwa wanataka kuwa na mwanzo mpya.

"kwa tukio hili, FARC tunataka wkuionyesha nchi na kwamba tunafunga ukurasa kwaajili ya historia ya taifa letu na kuanza kuandika historia mpya.Tunataka mtambue kuwa Amani ni jambo muhimu katika mioyo yetu,na kwamba sasa nguvu zetu zitaelekezwa katika ujenzi wa taifa letu na hiyo ndiyo ndoto yetu "

Kwa mjibu wa makubaliano ya mkabata uliowekwa,kundi la FARC kwa sasa limekubali kuingia katika mfumo wa kujibadili na kuwa kundi la harakati za kisiasa na kuachana na msimamo wa kuamini ukombozi kupitia silaha ambao limekuwa nao kwa miaka mingi hadi sasa

Mada zinazohusiana