Moto mkubwa wazuka katika jengo refu London

London
Image caption Jengo moja la ghorofa limeshika moto katika barabara ya Latimer, magharibi mwa jiji la London

Jengo moja la ghorofa limeshika moto katika barabara ya Latimer, magharibi mwa jiji la London, watu walio shuhudia tukio hilo wanasema,moto huo umeleta mshituko mkubwa hali iliyosababisha baadhi ya watu kushindwa kutoka katika makazi yao.

Hadi sasa moto huo unaendelea kuunguza jengo hilo vikosi vya uokoaji na zima moto takribani 200 vikiendelea na kazi hiyo.

Polisi wanmesema kuwa hadi sasa imebainika kuwa ni watu wawili tu ambao wameathirika na moshi wa moto huo na wanapata matibabu .

Mwandishi wa BBC Andy Moore aliyepo katika eneo la tukio kwa sasa anasema jengo hilo lina wasiwasi wa kuanguka wakati wowote.