Watu 12 wafariki wafariki baada ya moto kuteketeza jengo refu London

Grenfell Tower Fire
Image caption Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo

Watu 12 wamethibtiishwa kufariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London, polisi wa jiji hilo wamesema.

Idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.

Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, ambapo walioshuhudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada.

Zaidi ya watu 50 wanatibiwa hospitalini.

Mwandishi wa BBC alisema kuwa kulikuwa na hofu kuwa jengo hilo lingeporomoka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moshi uliweza kuonekana kutoka mbali

Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza.

Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sehemu kubwa ya jengo ilishika moto

Mwandishi wa BBC Andy Moore aliyekuwepo katika eneo la tukio alisema jengo hilo liikumbwa na wasiwasi wa kuanguka.

Image caption Takribani wazima moto 200 walishiriki kupambana nao.

Mada zinazohusiana