Mwanasheria mkuu Jeff Sessions akana kufanya mikutano ya siri na maafisa wa Urusi

Attorney General Jeff Sessions

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanasheria mkuu Jeff Sessions

Mwanasheria mkuu nchini Marekani Jeff Sessions amekana wakati wa kikao cha Seneti kuwa, hakufanya mikutano ya siri na maafisa Urusi kwenye hiteli huko Washington DC

Sessions pia aliiambia kamati hiyo ya Seneti kuwa madai kwamba alishirikiana na Urusi hayakuwa ya ukweli.

Bwana Sessions pia mara kwa mara alikataa kujibu maswali kuhusu mawasiliani ya kibinafsi na Rais.

Aliapa kuwa ataendelea kujitetea dhidi ya madai ya uongo.

Matamshi ya Bwana Sessions yanakuja baada ya mkuu wa FBI aliyefutwa kusema kuwa anamnia alifutwa sababu ya uhunguzi unaofanywa na FBI kuhusu Urusi kuingia uchaguzi wa Marekani.

Chanzo cha picha, European photopress agency

Maelezo ya picha,

Kikao cha Seneti

Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini Urusi iliingilia kati uchaguzi wa Marekani ili kumsaidia Donald Trump kuchaguliwa.

Kamati hiyo ya seneti pia inachunguza ikiwa maafisa wa kampeni ya Trump walishirikiana Urusi.

Bwana Sessions ambaye ni mwanasheria mkuu nchini Marekania, aliiambia kamati ya seneti kuwa hajajulishwa kamwe kuhusu Urusi kuingilia kati uchaguzi wa mwaka uliopita.