Watu watatu wauawa kwa kupigwa risasi Marekani

Polisi wanasema ulinzi umeimarishwa zaidi kwa sasa
Image caption Polisi wanasema ulinzi umeimarishwa zaidi kwa sasa

Polisi katika mji wa San Francisco wamesema watu watatu wameuawa katika shambulio la kufyatua risasi.

Mfyatuaji ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kampuni moja pia alifariki.

Polisi wanasema alijifyatulia risasi mwenyewe wakati wakijaribu kumkamata.

Image caption Watu wakiwa wanaondolewa katika eneo hilo

Watu wengine wawili walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Msemaji wa jeshi la polisi amesema kuwa tukio hilo halina uhusiano na ugaidi.