Watu tisa wauawa katika mlipuko Mogadishu

Mashuhuda wanasema gari hilo lilikuwa na mbio kali
Image caption Mashuhuda wanasema gari hilo lilikuwa na mbio kali

Takriban watu tisa wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari kulipuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Polisi wanasema gari lililokuwa na bomu hilo lililipuka wakati likielekea katika hoteli ya Posh Treats iliyopo katikati ya mji.

Mmoja wa mashuhuda amesema aliona miili kadhaa ikitapakaa baada ya tukio hilo.

Kundi la wapiganaji wa al-Shabaab limekiri kuhusika na shambulizi hilo.