Aliyempiga mbunge wa Republican risasi auawa Marekani

Police investigate a shooting scene after a gunman opened fire on Republican members of Congress during a baseball practice near Washington in Alexandria Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wakichunguza eneo la tukio

Mtu mwenye silaha ambaye aliwafyatulia risasi wabunge wa Republican wakati wakifanya mazoezi ya mchezo wa baseball mjini Washington DC ameuwa.

Kinara wa walio wengi bungeni Steve Scalise, ni mmoja wa wale waliojeruhiwa wakati wa kisa hicho cha mapema asubuhi katika hustani huko Alexandria , Virginia.

Mshambualiaji ambaye ni mzaliwa wa Illiois James T Hodgkinson, mwenye umri wa miaka 66, aliuawa baada ya ufyatulianaji wa risasi na polisi.

Waliojeruhiwa ni pamoja na polisi wawili.

Hodgkinson alikuwa amemfanyia kampeni mgombea urais wa Democratic Bernie Sanders.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mbuge aliyepiwa risasi Steve Scalise

Ukurasa wa Facebook ambao unaonekana kuwa wa Bwana Hodgkinsion, umejaa propaganda dhidi ya Republican na Trump.

Bwana Sanders ambaye ni Seneta wa Vermont amesema amehusunishwa na kitendo hicho cha Hodgkinson.

Rais wa Marekani Donald Trump ametaja shambulia hilo kuwa la kinyama.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wabunge 25 wwa Republican walikuw mazoezini

Trump alimtembelea bwana Scalise ambaye alipiwa risasi kwenye nyonga na yuko hali mahuti baada ya kufanyiwa upasuaji.

Hospitali ilisema kuwa Bwana Scalise alivunjika mifupa, na kupata majeraha ya viungo vya ndani na hivyo atahitaji upasuaji zaidi.

Haki miliki ya picha Illinois State's Attorney Office
Image caption James T Hodgkinson alikuwa mkaazi wa Illinois

Mada zinazohusiana