Trump achunguzwa kwa kuzuia sheria

Robert Mueller. File photo Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Robert Mueller is overseeing the investigation into Russia's alleged meddling and any Trump links

Rais wa Marekani Donald Trump anachungzuwa na mwanasheria maalum Robert Mueller, kwa kile kinachotajwa kuwa alizuia sheria, kwa mujibu wa gaezti la Washington Post.

Gazeti hilo linasema kuwa maafisa watatu wa vyeo vya juu wamekubali kuhojiwa na wachunguzi wa Bwana Mueller.

Wakili wa Bwana Trump walisema kuwa hatua ya FBI kifichua taarifa kwa gazeti hilo ni kitendo kibaya.

Bwana Muller anaongoza uchunguzi wa FBI kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016 na uhusiano wowote wa Trump kwa suala hilo.

Rais Trump mara kwa mara amekana kuwopo ushirikiano wowote na Urusi.

Siku ya Jumatano gazeti la washington post lilitaja hatua ya Bwana Muller kuchunguza mienendo ya Rais Trump kama hatua kubwa katika uchunguzi huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump

Maafisa ambao hawakutajwa walieleza gazeti hilo kuwa uchunguzi kuhusu Trumpo kuzuia sheria ulianza siku kadha baada ya Trump kumfuta mkuu wa FBI James Comey tarehe 9 mwezi Mei.

Kabla hajafutwa Bwana Trump alikuwa amepewa hakikisho kutoka kwa Bwana Comey kuwa sio yeye alikuwa akichunguzwa.

Hata hivyo Bwana Comey tangu wakati huo amedai kuwa Bwana Trump alikuwa amejitahidi kumshawishi aachane na uchunguzi dhidi ya mshauri wake wa masuala ya usalama Machael Flynn.

Bwana Flynn alifutwa mwezi Februari kwa kushindwa kufichua kiwango cha uhusiano wake na Sergei Kislyak, ambaye ni balozi wa Urusi nchini Marekani.