Shambulizi la kigaidi lawaua zaidi ya watu 18 mjini Mogadishu, Somalia

Security forces and an ambulance at the scene of the attack in Mogadishu. Photo: 14 June 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi vya Somalia vimefunga eneo hilo

Shambulizi la bomu la kujitoa mhanga na la bunduki katik hoteli moja na mgahawa kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, limewaua takriban watu 18.

Shambulizi hilo lilianza siku ya Jumatano jioni wakati waislamu walikuwa wakifungua siku yao ya kufunga ya mwezi mtukufu wa Ramadan

Wanamgambo kutoka kundi la al-Shabab waliwashikilia zaidi ya mateka 20 wakati waaufyatuaji wa risasi ambao kwa sasa umekwisha.

Kundi hilo lenye uhusiano na kundi al-Qaeda lilikiri kutekeleza shambulizi hilo lililofanyika mapema Alhamisi.

Shambulizi hilo lilianza mwendo wa saa mbili usiku wakati gari lililokuwa limejazwa milipuko lilishambulia hoteli hiyo ya kifahari karibu na mgahawa, ambalo ndilo eneo pekee mjini Mogadishu lililo na discco.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko huo uliweza kuonekana kwa mbali kutoka hoteli iliyoshambuliwa

Kisha watu wenye bunduki wakaingia mgahawa uliokuwa karibu na kuwashika watu mateka.

Wenyeji wanasena walisikia sauti za risasi usiku kucha lakini hali kwa sasa imetulia.

Pia kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kuwa washambuliaji walikuwa wamevalia sare za polisi.

Vikosi kutoka kwa Muungano wa Afika viliwatimua wanamgambo wa al-Shabab kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011, lakini eneo kubwa la nchi bado liko mikononi mwa wanamgambo hao.

Image caption Somalia

Mada zinazohusiana