Risasi yampiga kimakosa na kukwama kwenye shingo la mwandishi wa habari Ufilipino

Tweet reads "Lucky" and picture shows an X ray image of a bullet lodged in a neck, between two vertebrae level with the jaw Haki miliki ya picha @adharves
Image caption Adam Harvey alidhani amegongwa na kitu kama mpira wa kriketi

Mwandishi mmoja wa habari amepigwa na risasi kimakosa shingoni wakati akifuatilia mapigano nchini Ufilipino.

Adam Harvey anayefanya kazi na kituo cha ABC alichapisha picha ya X-ray katika mtandao wa Twitter ya risasi iliyokwama ndani ya shingo lake.

Hata hivyo jera hilo sio la kumtishia maisha, mkurugenzi wa ABC alisema.

Mapigano yalianza baada ya wanamgambo wanaotangaza kulitii kundi la Islamic State, kuthibiti baadhi ya maeneo ya mji wa Marawi katika kisiwa cha mindanao mwezi Mei.

Kuna ripori kuwa baadhi ya wakazi bado wamekwama mjini humo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bwana Harvey

Mwanasiasa mmoja amesema kuwa wale ambao wamefanikiwa kuondoka wameripoti kuona maiti nyingi za watu waliouawa kwenye mapigano kati ya wanamgambo na vikosi vya usalama.

Bwana Harvey anasema alikuwa akiinama kuchukua chakula kutoka kwa gari akiwa amevalia mavazi ya kujinga dhidi ya risasi, wakati aligonjwa na kitu alichohisi kuwa ni kama mpira wa kriketi.

Alipewa huduma ya kwanza akifikiri kuwa labda alikuwa amegongwa na ganda la risasi, lakini wakati aliamua kutibiwa picha za X-ray zilionyesha alikuwa amepigwa risasi.