Waziri mkuu wa Australia arekodiwa akimkejeli rais wa marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull

Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull amerekodiwa akimkejeli rais wa Marekani Donald Trump katika mkanda wa video ulionyeshwa na chombo cha habari.

Bwana Turnbull alirekodiwa akizungumza katika mkutano wa wanahabari katika jumba la bunge siku ya Jumatano usiku.

Mkutano huo wa habari huwa habari zake haziripotiwi , lakini mhariri wa maswala ya kisiasa wa kituo cha televisheni cha Nine cha Australia amesema aliamua kuvunja amri hiyo na kutangaza mkutano huo hadharani.

Bwana Turn Bull amesema ripoti hiyo ilikuwa ''ukiukaji wa imani''

Bwana Trump na Turnbull hivi majuzi waliimarisha mahusiano yao baada ya tofauti kuibuka baina yao hapo mwanzo.

Hapo awali walikuwa na mazungumzo makali ya simu dhidi ya Bwna Trump kwa ulegevu wa kukubali mpango wa kuwakubali wakimbizi 1,200 kutoka kambi ya waliokamatwa ya Australia.

Lakini mwezi uliopita viongozi hao wawili walikutana mjini New York , ambapo Bwana Trump alielezea uhusiano wao kuwa ''mzuri''.

Mhariri wa Kituo cha televisheni cha Nine Laurie Oakes , aliyeripoti taarifa hiyo , amesema yeye hakuhudhuria mkutano huo , lakini sauti ya filamu hiyo ilijitokeza na video sawia na hiyo ilikuwa imechapishwa kwenye mtandowa Instagram.

Muajiri wake, amesema Bw Oakes, hakubaliani kwamba ripoti zozote zinazihudhuriwa na wanahabari hazistahili kutangazwa.

Australia ni miongoni mwa nchi ambazo ni rafiki wa karibu wa Marekani.

Majeshi wa nchi hizo mbili yameungana katika mapingano ya pamoja katika vita vikubwa vilivyoshuhudiwa ikijumuisha Iraq na Afganistan.