Mlipuko wakumba shule ya chekechea China

Chombo cha habari cha Xinhua kimesema kuwa mlipuko huo ulitokea nje ya shule hiyo katika kaunti ya Fengxian mkoa wa mashariki wa Jiangsu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chombo cha habari cha Xinhua kimesema kuwa mlipuko huo ulitokea nje ya shule hiyo katika kaunti ya Fengxian mkoa wa mashariki wa Jiangsu

Watu saba wameripotiwa kufariki huku wengine 59 wakijeruhiwa katika mlipuko uliofanyika katika shule ya chekechea nchini China, kulingana na chombo cha habari cha serikali.

Chombo cha habari cha Xinhua kimesema kuwa mlipuko huo ulitokea nje ya shule hiyo katika kaunti ya Fengxian mkoa wa mashariki wa Jiangsu.

Haijulikani ni watoto wangapi walioathiriwa na mlipuko huo.

Sababu ya mlipuko huo haijulikani.

Unaaminika kutokea wakati wazazi walipokuwa wakiwachukua watoto wao nyakati za jioni.

Picha ambazo hazijafanyiwa uhakiki zilionyesha watu wazima waliokuwa wakivuja damu huku watoto wakiwa wamelala ardhini.

Kanda ya video ilionyesha watu waliojeruhiwa wakiwabeba watoto waliokuwa wakilia huku mwanamke mmoja aliyevalia nguo zilizochomeka akionekana kupepesuka.

Watu wawilki waliuawa papo hapo huku wengine watano wakifariki kutokana na majeraha kulingana na Xhinua.

Tisa ya waliojeruhiwa wamedaiwa kuwa katika hali mahututi.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa wameanzisha uchunguzi .

Tovuti ya habari ya China Sohu ilimnukuu mmiliki mmoja wa duka akisema mlipuko mkubwa umesikika ambao anadhani huenda ulisababishwa na kulipuka kwa gesi katika mgahawa mmoja wa chakula.