Erdogan kuwalinda walinzi waliopiga waandamanaji Washington

Walinzi wa Erdogan wakiwashambulia Raia wa Uturuki waishio Marekani
Image caption Walinzi wa Erdogan wakiwashambulia Raia wa Uturuki waishio Marekani

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema atafanya kila liwezekanalo kushughulikia kuondolewa kwa kibali cha kukamatwa kwa walinzi wake 12 ambao walionekana kuwapiga waandamanaji mjini Washington.

Tukio hilo lilitokea nje ya ubalozi wa Uturuki mwezi uliopita.

Picha za video zinaonyesha zinaonyesha walinzi wa Erdogan wakiwapiga mateke baadhi ya waandamanaji huku Rais Erdogan akishuhudia tukio hilo.

Image caption Rais Erdogan amesema walinzi wake walikuwa wakifanya kazi yao

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa walinzi hao watakamatwa iwapo watarejea nchini humo wakati wowote.