Mpenzi wa jinsia moja achaguliwa waziri mkuu Serbia

Ana Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ana Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic.

Rais wa Serbia amemteua mwanamke ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa waziri mkuu katika jimbo la kihafidhana la Balkan.

Ana Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic.

Kuidhinishwa kwake na bunge kutakuwa rasmi kwa kuwa chama chake na washirika wake wana wajumbe wengi.

Miaka michache iliopita uteuzi wa mtu wa mapenzi ya jinsia moja usingedhaniwa.

Lakini Serbia inayosubiri kujiunga na bara Ulaya imeonyesha ithibati kwamba kuna ongezeko la uvumilivu miongoni mwa raia wa eneo hilo.

Hatahivyo kiongozi wa chama kidogo katika muungano wa rais huyo Dragan Markovic Palma wa muungano wa Serbia alisema kuwa bi Brnabic ''sio chagua lake la waziri wake mkuu''.

Bi Brnabic atajiunga na idadi ndogo ya mawaziri wakuu ambao ni wapenzi wa jinsia moja ili kuongoza serikali barani Ulaya ikiwemo Leo Varadkar wa Jamhuri ya Ireland na Xavier Bettel wa Luxenbourg.

Wadhfa wa waziri mkuu katika utawala huo utakuwa na uwezo hafifu.