Waliofariki mkasa wa moto London wafika 30

Malkia Elizabeth Haki miliki ya picha PA
Image caption Malkia Elizabeth ametembelea kituo cha misaada ambacho kinawasaidia manusura wa mkasa huo wa moto.

Polisi wamethibitisha kwamba idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa wa moto katika jumba la Grenfell Tower magharibi mwa London imefikia 30.

Bado kuna watu wengi ambao hawajulikani walipo.

Kamanda wa polisi Stuart Cundy amesema inaaminika kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka, lakini kwa sasa ni vigumu sana kubaini ni watu wangapi ambao hawajulikani walipo.

Hii ni kwa sababu huenda jamaa wamepiga ripoti mara kadha, kila mmoja kivyake, kuhusu jamaa zao ambao hawajui waliko.

Amesema polisi watachunguza kubaini iwapo kulitendwa makosa ya jinai.

Malkia Elizabeth na Mwanamfalme William walitembelea kituo cha misaada ambacho kinawasaidia manusura wa mkasa huo wa moto.

Haki miliki ya picha Getty Images

Waziri Mkuu Theresa May naye amezungumza na majeruhi hospitalini, baada yake kukosolewa kwamba hakuzungumza na wakazi alipozuru eneo la mkasa Alhamisi.

Moto huo ulizuka mwendo wa saa moja usiku, usiku wa kuamkia Jumatano.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maafisa wamesema hawatarajii kuwapata manusura

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii