Cuba yalaani hatua ya Trump kuiwekea vikwazo upya

Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump akiongea huko Miami

Serikali ya Cuba imelaani vikali hatua ya Rais Trump kuiwekea upya vikwazo vya usafiri na biashara taifa hilo baada ya utawala wa Barak Obama kulegeza sheria hiyo, katika harakati ya kuboresha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ubalozi wa Marekani miji Havana

Akiwahutubia wamarekani wenye asili ya Cuba mjini Miami, Trump amesema hatua yake imechangiwa na rekodi ya Cuba ya Ukiukaji wa haki za binadamu hasa, wakati wa utawala wa kidikteta wa Fidel Castro.

Amesema sera hiyo mpya itatilia mkazo sheria juu ya usafiri na kutuma fedha nchini humo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wakitembea mjini Havana

Havana hata hivyo imeskitishwa na uamuzi huo na kuongeza kuwa unarudisha nyuma ushirikiano wa kimaendeleo baina ya mataifa hayo na kwamba Marekani haiwezi kuishauri Cuba juu ya masuala ya haki za binadamu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Obama na rais wa Cuba Raul Castro 2016