AU yataka Djibout na Eritrea kuwa watulivu

AU yataka Djibout na Eritrea kuwa watulivu
Image caption AU yataka Djibout na Eritrea kuwa watulivu

Muungano wa Afrika AU imetoa wito wa utulivu baina ya Djibouti na Eritrea huku mzozo wa mpaka bainia ya mataifa hayo mawili ukinukia.

Hapo jana,Djibouti ililaumu taifa jirani la Eritrea kwa kupeleka vikosi vyake katika eneo la mpakani linalo zozaniwa baada ya Qatar kuondoa walinda amani wake katika eneo hilo.

Doha ilichukuwa ya hatua hiyo baada ya kuibuka madai kwamba mataifa hayo ya Afrika mashariki yanaunga mkono Saudi Arabia katika mzozo wake na Qatar.

Djibouti na Eritrea zilipigana mwaka 2008 juu ya mzozo wa pakani hadi pale Qatar ilipoingilia kati mzozo huo na kupeleka kikosi chake kulinda amani katika eneo hilo.