Mlipuko wa bomu wauwa 3 Colombia

Watu waliondolewa kwa haraka katika eneo la Centro Andino mall, baada ya mlipuko kutokea Haki miliki ya picha NATALIO COSOY / BBC
Image caption Watu waliondolewa kwa haraka katika eneo la Centro Andino mall, baada ya mlipuko kutokea

Wanawake watatu wameuwawa, katika kile wakuu nchini Colombia wanasema kuwa, shambulio la kigaidi katika mji mkuu Bogota.

Mlipuko huo ulitokea katika soko moja la biashara la Zona Rosa, katika mji mkuu Bogota.

Watu wengine 11 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Meya wa Bogota, Enrique Penalosa, amesema kuwa mmoja wa wanawake aliyefariki anatoka Ufaransa.

Viongozi Colombia watia saini makubaliano ya amani

Maandamano nchini Colombia

Waasi 12 wa Farc wabadilika na kuwa raia Colombia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wakipiga doria nje ya maduka hayo

Wakuu wanaamini kuwa mlipuko huo ulitokea ndani ya choo cha wanawake, baada ya bomu dogo kulipuka.

Mlipuko huo ulitokea Jumamosi alasiri wakati wa shughuli nyingi, katika soko hilo la kibiashara, pale lilikuwa limejaa wateja, waliokuwa wakinunua bidhaa za siku kuu ya kina baba Duniani-- ambayo inasherehekewa leo siku ya Jumapili, Juni 18.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Santos akiwa katika maeneo hayo ya maduka ya Andino

Haijabainika ni nani au kundi lipi, lilitekeleza shambulizi hilo.