Beyonce Knowles ajifungua pacha

Beyonce amejifungua pacha
Image caption Beyonce amejifungua pacha

Nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani Beyonce amejifungua mapacha kulingana na vyombo vya habari nchini Marekani.

Vyombo vya habari vya Entertainment Weekely, Us Weekly na People Magazine vimethibitisha habari hizo lakini tarehe ya kuzaliwa na jinsia ya watoto haijajulikana.

Beyonce ambaye ni mkewe mwanamuziki wa mtindo wa Rap Jay Z alitangaza kwamba ni mjamzito katika picha ya Istangram mnamo mwezi Februari ambapo ni picha iliopendwa mno katika historia ya mtandao huo.

Haki miliki ya picha Beyonce.com
Image caption Beyonce Knowles na mwanawe Blue Ivy katika picha moja baada ya kutangaza kuwa ni mjamzito

Wawili hao tayari wana mwana wa kike, kwa jina Blue Ivy aliye na umri wa miaka mitano.

Hakujakuwa na tangazo rasmi kuhusu kujifungua huko kutoka kwa Beyonce na Jay Z mwenyewe.

Picha nyengine zilizochapishwa na Beyonce baada ya kutangaza kuwa ni mjamzito ziliomuonyesha akiogelea chini ya maji, akiwa katika maua huku akiwa amekaa uchi ndani shada la maua.

Haki miliki ya picha Beyonce.com
Image caption Picha iliomuonyesha Beyonce akiogelea chini ya maji wakati akiwa mjamzito

Katika picha moja mwimbaji huyo wa wimbo 'Lemonade' alisimama akiwa uchi na kushikilia tumbo lake na mkono mmoja na mwengine akishikilia titi lake , mbele ya kichwa cha kiongozi wa zamani wa Msiri.