Serikali ya Sudan yaombwa kutangaza janga la kipindupindu

Kituo cha kutibu ugonjwa wa Kipindupindu Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Kituo cha kutibu ugonjwa wa Kipindupindu

Tawi la muungano unaotetea maslahi ya madaktari wa Sudan, lililoko Uingereza, Limeiomba serikali ya Khartoum kutangaza mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kuwa janga kubwa nchini humo .

Mamlaka kuu nchini Sudan, imekubali kuwa, takriban watu 280 wamefariki, huku wengine elfu 15 wakiathirika na ugonjwa huo.

Lakini wamepinga kuwa watu hao walikufa kutokana na kipindupindu.

Hisham el-Khidr, Rais wa muungano huo wa madaktari nchini Uingereza, anasema kuwa sekta ya afya imesambaratika