Mwelekezi wa filamu ya Rocky na Karate Kid afariki

John G. Avildsen, mshindi wa tuzo za Oscar kwa kuwa mwelekezi wa filamu ya Rocky na The Karate Kid Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption John G. Avildsen, mshindi wa tuzo za Oscar kwa kuwa mwelekezi wa filamu ya Rocky na The Karate Kid

John G. Avildsen, mshindi wa tuzo za Oscar kwa kuwa mwelekezi wa filamu ya Rocky na The Karate Kid amefariki akiwa na umri wa miaka 81.

Mwana wa Avildsen Anthony aliambia vyombo vya habari nchini Marekani kwamba mtayarishaji huyo wa filamu alifariki kutokana na saratani katika hospitali ya Sinai Medical Senter mjini Los Angeles.

Rocky ilioigizwa na Sylvester Stallone kama bondia aliyejitoa katika ufukara na kuwa tajiri ilikuwa filamu iliouzwa sana mwaka 1976 licha ya kuwa na bajeti ya chini.

Ilishinda tuzo la Oscar kwa kuwa picha bora huku mwelekezaji Avildsen akijishindia tuzo la uelekezaji bora.

Stallone aliyeandika filamu hiyo alimpatia sifa nyingi mwelekezaji wake.

Aliandika ujumbe huu katika mtandao wa Istagram: ''RIP nina hakika hivi karibuni utaanza kuelekeza filamu ukiwa peponi''.

Avildsen pia alielekeza filamu ya Karate Kid iliotolewa mwaka 1984 pamoja na Karate Kid awamu ya pili 1986 na Karate Kid awamu ya tatu 1989.