Misaada ya chakula haiwafikii walengwa

Nigeria
Image caption Yemi Osinbajo mwenye kofia nyeusi akiwa pamoja na Kashim Shettima

Maofisa nchini Nigeria wamearifu kwamba nusu ya chakula cha msaada kilichokuwa kimepelekwa kwa watu waliosambaratishwa kutoka katika makaazi yao na kundi la wana mgambo wa kiislam hakijawafikia walengwa.Idadi ya watu hao inakadiriwa kufikia milioni tatu katika kipindi cha miaka nane ya uasi wa wapiganaji wa Boko Haram

Msemaji wa kaimu rais wa Nigeria, Yemi Osinbajo, amesema kwamba mfumo mpya umezinduliwa mapema mwezi huu, na kuleta mabadiliko makubwa katika usambazaji misaada ya kibinaadamu, huku dhana ya kuibwa kwa misaada hiyo na kwenda katika mikono isiyostahili ikirindima.

Kwa sasa, maelfu ya polisi na wanajeshi wamechukua hatua ya kusindikiza magari hayo yenye kusambaza misaada ya chakula, ili iweze kufika katika maeneo stahiki na kuwapa wenye uhitaji.

Zaidi ya magari ya misaada milioni moja yaliyosheheni nafaka yako njiani kuelekea Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. Watu milioni moja unusu wako katika njaa kuu.

Nao wapiganaji wa Boko Haram wanaendelea na mashambulizi bila kukoma, pamoja na mashambulizi na wakati mgumu wanaokabiliana nao kutoka katika jeshi la Nigeria.