Marekani yatoa majina ya wanajeshi waliouwawa baharini

The USS Fitzgerald, damaged by colliding with a Philippine-flagged merchant vessel, on 17 June 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ajali hiyo ilisababisha shimo kubwa kweny meli ya kijeshi

Marekani imetangaza majina ya wanajeshi wake 7 ambao waliuawa wakati meli yao iligongana na ile ya mizigo katika eneo la bahari ya Japan siku ya Jumamosi.

Wanjeshi hao walipatikana katika maneo yaliyokuwa yamefurika maji ndani ya meli hiyo ya kivita ya USS Fitzgerald.

Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa kwenye kisa hicho ambacho kilitokea karibu na mji wa bandari wa Yokosuka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meli hiyo kwa sasa imepelekwa huko Yokosuka

Wengi wa wanajeshi walikuwa wamelala wakati meli hizo ziligongana. Marekani inasema kuwa inafanya uchunguzi.

Wanajeshi hao waliripotiwa kutoweka baada ya ajali hiyo.

Kamanda wa meli ya kijeshi Joseph P Aucoin aliwaambai waandishi wa habari kuwa ajali hiyo ilisababisha shimo kubwa kwenye meli ya kijeshi.

Wanajehsi hao saba ni pamoja na:

  • Dakota Kyle Rigsby, 19
  • Shingo Alexander Douglass, 25
  • Ngoc T Truong Huynh, 25
  • Noe Hernandez, 26
  • Carlos Victor Ganzon Sibayan, 23
  • Xavier Alec Martin, 24
  • Gary Leo Rehm Jr, 37
Image caption Ramani inayoonyesha eneo la ajali