Wanaume watatu waiba maparachichi ya $300,000

Bei ya maparachichi imepanda sana duniani Haki miliki ya picha PA
Image caption Bei ya maparachichi imepanda sana duniani

Wanaume watatu katika jimbo la California nchini Marekani wamekamatwa na kuzuiliwa, wakituhumiwa kuiba maparachichi ya thamani ya $300,000 (£234,770) .

Kuongezeka kwa hitaji la matunda hayo duniani mwezi Mei kulisababisha bei ya maparachichi kupanda sana.

Polisi wanasema hilo huenda liliwafanya wanaume hao kushawishika kuiba matunda hayo kutoka kwa kampuni ya matunda ya Oxnard walipokuwa wanafanya kazi.

Afisi ya liwali wa wilaya ya Ventura imesema Carlos Chavez, Rahim Leblanc, na Joseph Valenzuela walikamatwa Jumatano.

Walikuwa wamefanya kazi katika Mission Produce, moja ya kampuni zinazoongoza duniani kwa usambazaji wa maparachichi, kwa miaka kadha.

Polisi wanaamini watatu hao wamekuwa wakiiba matunda hayo, kwa miezi kadha, na kuwauzia wateja ambao hawakuwa na ufahamu kwamba yalikuwa ya wizi.

Rais wa kampuni hiyo, Steve Barnard, anasema sanduku moja ya maparachichi kawaida huuzwa $50, lakini wanaume hao walikuwa wanauza nusu ya bei hiyo.

Bei ya Maparachichi ya Hass

(Bei ya rejareja Marekani)

$1.27

tunda moja Aprili 2017

  • $0.98 Aprili 2016

Getty

"Hitaji la matunda hayo limeongezeka. Kila mtu anapenda maparachichi," Sajenti John Franchi wa afisi hiyo ya liwali aliambia gazeti la LA Times.

"Tunachukulia visa kama hivi vya wizi kwa uzito sana. Ni zao muhimu sana hapa na California."

Mataifa yanayozalisha maparachihi kwa wingi zaidi duniani
1. Mexico
2. Jamhuri ya Dominika
3. Colombia
4. Peru
5. Indonesia

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii