Wanaume 4 watoroka jela kupitia njia ya ardhini Indonesia

The four men escaped by digging a tunnel from the prison clinic to an outside wall. Haki miliki ya picha ABC
Image caption Wanaume hao wanaaminiwa kuitoroka jela kupitia njia ya chini ya radhi

Polisi nchini Indonesia wanawatafuta wanaumume wanne raia wa kigeni ambao walitoroka jela mjini Bali wakitumia njia ya chini ya ardhi.

Wanaume hao walitambliwa kama Shaun Edward Davidson kutoka Australia, Dimitar Nikolov raia Bulgaria, Raia wa India Sayed Muhammad na raia wa Malaysia Tee Kok King.

Mkuu wa jela la Kerokoban alisema anaamini wanaume hao bado wako kisiwani humo.

Haki miliki ya picha ABC
Image caption Picha na wanaume hao zimesambwazwa kote nchini Bali

Magereza nchini Indonesia hukumbana na watu wengi wanaukamatwa kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya na visa vya kutoroka jela ni vingi.

Wanaume hao wanaaminiwa kuitoroka jela kupitia njia ya chini ya radhi

Ilibanika kuwa watu hao hawakuwepo Jumatatu wakati ya ukaguzi wa kawaida.