Korea Kaskazini: Marekani iliwapora wanadiplomasia wetu

People head towards departures at John F Kennedy Airport in 2016 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Msemaji wa taifa hilo lilijitenga alisema kuwa maafisa wake waliporwa mizigo yao katika uwanja wa ndege wa JF Kenedy siku ya Ijumaa.

Korea kaskazini imelaumu mamlaka nchini Marekani kwa kuwapora wanadiplomasia wake katika uwanja wa ndege mjini New York.

Msemaji wa taifa hilo lilijitenga alisema kuwa maafisa wake waliporwa mizigo yao katika uwanja wa ndege wa JF Kenedy siku ya Ijumaa.

Shirika la habari nchini Korea Kaskazini KCNA, lilisema kuwa kisa kilionyesha kuwa marekani ni taifa jambazi.

Ikulu ya Marekani hata hivyo haijasema lolote.

Wanadiplomasia wa Korea Kaskazini wanadaiwa kurejea kotoka mkutano wa Umoja wa Mataifa wakati kisa hicho kilitokea

Kisa hichi cha hicho huenda kikawa msumari wa moto kwenye kidonda kwa uhusiano ulioharibika kati ya nchi hizo mbili.

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilimrejesha mwanafunzi raia wa Marekani Otto Wambier kwa afamilia yake, baada ya zaidi ya mwaka moja tangu hukumiwe kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu.

Bwana Warmbier alikuwa amepoteza fahamu na alikuwa na madhara makubwa kwenye ubongo.